MAKAMU wa Rais Dk Philip Mpango anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa Kimataifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi-COP29.
Mkutano huo umepangwa kufanyika Novemba 11 hadi 22 katika mji mkuu wa Azerbaijan, Baku.
SOMA: Mikakati yawekwa kukabili mabadiliko ya tabia nchi
Kauli mbiu ya mkutano huo ni “Kutumia fursa za biashara ya kaboni kuchagiza matumizi ya nishati safi ya kupikia pamoja na vyanzo vya nishati mbadala.”