Dk Mwinyi ateua kamishna, wakurugenzi

ZANZIBAR – RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amefanya uteuzi wa kamishna na wakurugenzi katika wizara na taasisi za serikali.

Amemteua Omar Said Omar kuwa Kamishna wa Usimamizi wa Sera za Ununuzi wa Umma katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.

Kabla alikuwa Mkurugenzi wa Kujenga Uwezo na Huduma za Ushauri katika Mamlaka ya Ununuzi na Uondoshaji wa Mali za Umma (ZPPDA). Pia, amemteua Suleiman Saleh Haji kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa ZPPDA.

Kabla alikuwa Meneja wa Masuala ya Ununuzi wa Kampuni ya Maendeleo ya Petroli ya Zanzibar (ZPDC). Amemteua Rajab Uweje Yakoub kuwa Mkurugenzi Idara ya Uendeshaji na Utumishi katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango.

SOMA: Biteko awabana watendaji utoshelevu umeme

Kabla alikuwa Ofisa Mwandamizi Utawala katika Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango. Aidha, Issa Sarboko Makarani ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti katika Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi.

Issa ni mstaafu utumishi wa umma. Makame Salum Ali ameteuliwa Mkurugenzi wa Idara ya Mipango, Sera na Utafiti katika Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.

Kabla alikuwa Ofisa Mwandamizi wa Tume ya Mipango Zanzibar.

Habari Zifananazo

Back to top button