Filamu ya “The Royal Tour” yazaa matunda

FILAMU ya Royal Tour ya kutangaza vivutio vya kitalii imeanza kuzaa matunda, kwani katika kipindi Januari hadi Disema mwaka jana idadi ya watalii walioingia nchini iliongezeka na kufikia watalii zaidi ya milioni 1.4 ingilinganishwa na watalii 922,692 mwaka 2021 ni ongezeko la asilimia 57.7

Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi Takwimu na Uchumi nchini, Daniel Masolwa amesema hayo Agosti 8, 2023 na kusema kuwa idadi hiyo iliifanikishia serikali kuingiza Dola zaidi ya milioni 2.5 ikilinganishwa na Dola zaidi ya milioni 1.3 zilizoingizwa mwaka 2021.

Masolwa alisema wastani matumizi ya mtalii mmoja kwa siku walioingia mwaka jana iliongezeka hadi Dola 214 ikilinganishwa na Dola 199 mwaka 2021 na hiyo ni sawa na ongezeko la asilimia 92.9.

Alisema watalii wengi waliofika nchini mwaka jana ni kutoka nje ya Bara la Afrika ambao ni pamoja na Marekani watalii 100,600, Ufaransa watalii 100,371, Ujermani watalii 67,718, Uingereza watalii 60,116 na Poland watalii 46,431.

Alisema katika watalii waliokuja mwaka jana kutoka Bara la Afrika ni pamoja na Kenya watalii 166,324, Burundi watalii 100,851, Zambia watalii 46,787, Malawi watalii 44,438 na Rwanda watalii 44,288.

Masolwa alisema pia katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu idadi ya watalii imezidi kuongezeka zaidi na katika kipindi hicho watalii imeongezeka tofauti na mwaka jana kwani watalii 759,327 waliingia katika kipindi hicho ikilinganishwa na mwaka jana watalii 575,397 waliingia katika muda huo mwaka jana na hiyo ni ongezeko la asilimia 31.9.

Alisema watalii wengi walioingia nchini katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu ni kutoka nje ya Bara la Afrika na kipindi hiki Marekani iliendelea kuongoza kwani iliingia watalii 51,674,Ufarasa watalii 48,696 ,Ujermani watalii 39,789, Uingereza watalii 29,770 na Italia watalii 29,554.

Aidha watalii walioingia nchini katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu kutoka nchi za Bara la Afrika walitoka katika nchi za Kenya watalii 93,488, Burundi watalii 47,418 , Rwanda watalii 26,899, Zambia watalii 25,372 na Uganda watalii 20,727 walikuja nchini kutalii katika vivutio mbalimbali vilivyoko katika hifadhi.

Masolwa alisema kuwa watalii wengi waliokuja nchini kutalii mwaka jana na mwaka huu tafiti za ofisi yake zinasema kua walipata taarifa kupitia uhamashishaji wa serikali uliofanywa na kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na filamu ya Tanzania ‘’The Royal Tour”.

Alisema Serikali itaendelea kutangaza zaidi vivutio vya utalii nje ya nchi kwa kuwa bado kuna fursa kubwa ya kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea Tanzania na watalii wengi walifika nchini kwa lengo la kupumzika na idadi kubwa ya watalii waokuja nchini kutalii ni utalii wa wanyamapori na utalii wa ufukweni.

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button