Halmashauri zahimizwa ukaguzi bidhaa za chakula, vipodozi

KIGOMA: Halmashauri za Mkoa Kigoma zimetakiwa kufanya ukaguzi kwa wafanyabiashara wanaojishughulisha na biashara za chakula na vipodozi ili kuhakikisha wanafuata sheria na taratibu.
Ofisa Biashara wa Mkoa Kigoma, Moshi Ndimuligo amesema hayo wakati wa kikao cha tathmini baina ya maofisa wa Shirika la Viwango (TBS) Kanda ya Magharibi na maofisa biashara wakaguzi wa bidhaa za chakula na vipodozi kutoka Halmashauri za Mkoa Kigoma.

Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho, Moshi amesema kuwa tathmini inaonyesha kuwa kumekuwa na mwenendo wa kusuasua wa ukaguzi kwa wazalishaji na wafanyabiashara wa bidhaa za vyakula na vipodozi sambamba na kutotekelezwa kikamilifu kwa usajili wa majengo yanayohusika na uzalishaji wa bidhaa za vyakula na kwamba haali hiyo ni hatari kubwa kwa afya za wananchi.
Ofisa Biashara huyo amesema kuwa halmashauri zimekasimiwa kazi ya kufanya ukaguzi, usajili na ukusanyaji wa mapato ya maeneo yanayohusika na uzalishaji na biashara ya chakula na vipodozi lakini maifisa waliokabidhiwa jukumu la kusimamia kazi hiyo hawajatimiza wajibu wao kikamilifu huku kamati za halmashauri zinazohusikaa na ukaguzi huo zikiwa hazikutani kulingana na kalenda na utekelezaji wa majukumu yao.

Awali akizungumza katika mkutano huo Kaimu Meneja wa Kanda ya Magharibi wa Shirika la Viwango (TBS),Hamisi Seleleko aalisema kuwa kumekuwa na utekelezaji duni wa mpango wa kusajili majengo yaanayohusika na uzalishaji wa bidhaa za vyakula ambapo kuanzi mwezi Julai mwaka jana hadi kufikia mwezi Desemba mwaka jana liliwekwa lengo la kusajili majengo 1555 lakini kwa kipindi hicho ni majengo 235 tu yalisajiliwa.
Seleleko amesema kuwa kutokana na utekelezaji huo duni kiasi asilimia 15 ya mapato ya usajili wa majengo ya nayojishughulisha na bidhaa za vyakula zilizokuanywa katika lengo la kukusanya kiasi cha Sh milioni 31.




Sauti ya Mungu
I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com
I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com
Sauti ya Mungu
Sauti ya Mungu.
Sauti ya Mungu.