NI ushindi pekee utakaoiwezesha timu ya taifa ya mpira wa miguu ‘Taifa Stars’ katika mchezo wa mwisho wa makundi kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON 2025) leo.
Mchezo huo muhimu kwa Stars wa kundi H utafanyika kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam huku mashabiki wakiruhusiwa kuingia uwanjani bila kiingilio.
SOMA: Taifa Stars katika mtihani kufuzu AFCON leo
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Septemba 10 kwenye uwanja wa Yamoussoukro, Ivory Coast Stars ilishinda kwa mabao 2-1.
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DR Congo, inaongoza kundi H ikiwa na pointi 12 baada ya michezo mitano ikifuatiwa na Guinea yenye pointi tisa huku Taifa Stars ikishika nafasi ya tatu kwa kukusanya pointi saba wakati Ethiopia ina pointi moja mwisho wa msimamo.
Michezo mingine ya kufuzu AFCON inayofanyika leo ni kama ifuatavyo:
KUNDI C
Misri vs Botswana
Mauritania vs Cape Verde
KUNDI G
Ivory Coast vs Chad
Sierra Leone vs Zambia
KUNDI H
DR Congo vs Ethiopia
KUNDI I
Guinea-Bissau vs Msumbiji
Mali vs Eswatini
KUNDI J
Cameroon vs Zimbabwe
Kenya vs Namibia
KUNDI K
Congo vs Uganda
Afrika Kusini vs Sudan Kusini
KUNDI L
Senegal vs Burundi