Eng. Hersi anyakua tuzo Afrika

PARIS : RAIS  wa Timu ya mpira wa miguu,Young Africans SC na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vilabu Afrika, Eng. Hersi Ally Said ameshinda Tuzo ya mwanamichezo mwenye mchango katika maendeleo ya mpira wa miguu Barani Afrika katika tuzo za Nigeria-France Sports Awards, zilizofanyika  jijini Paris, Ufaransa.

Balozi wa Tanzania Nchini Ufaransa, Ali Jabir Mwadini, alikabidhiwa tuzo hiyo kwa niaba ya Eng. Hersi na kuelezea kuwa kwa kutambuliwa kwa mchango na juhudi za Eng. Hersi katika kukuza na kuendeleza mchezo wa mpira wa miguu nchini Tanzania na Barani Afrika.

Eng. Hersi ameonesha uongozi bora katika Young Africans SC, akichangia kwa kiasi kikubwa katika mafanikio ya Timu na kukuza vipaji vya wachezaji.

Advertisement

Tuzo hiyo inathibitisha mchango wake katika maendeleo ya michezo na ushirikiano wa kimataifa katika sekta hiyo, huku inaashiria umuhimu wa viongozi wa michezo katika kuleta maendeleo katika jamii.

SOMA: Hersi: Aziz Ki anabaki