Huduma za kibingwa kutolewa Sabasaba

DAR ES SALAAM: TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imesema itafanya kliniki maalum ya huduma za kibingwa bobezi ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu katika maonesho 49 ya biashara ya kimataifa maarufu kama Sabasaba kwa gharama nafuu.

Kliniki hiyo maalum itaanza Mei 28 hadi Julai 13,2025 katika banda namba 12 katika vinjwa vya Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Meneja Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi amesema kuwa gharama ya kumuona daktari bingwa itakuwa shilingi 5,000 na kipimo cha ultra sound kitakuwa Sh 10,000.

“Wananchi watahudumiwa pale kwenye banda letu,tofauti na miaka mingine ambapo tulikuwa tukionesha huduma zetu tunazozitoa MOI tumeona ni vyema kuzisogeza huduma zetu kwa wananchi,”amesisitiza.

Huduma za kibingwa zafika kanda ya kati

Mvungi ameeleza kuwa katika sabasaba zilizpopita waliweza kuhudumia watu 1000 hadi 1500 hivyo kwa wakati huu wanatarajia kuhudumia watu zaidi ya 2000 na kuendelea.

Kwa upande wake, daktari bingwa mbobezi wa upasuaji wa mifupa MOI, Dk Tumaini Minja amesema huduma zitakazotolewa ni mazoezi tiba na elimu ya mitindo bora ya maisha ili kujiepusha na maumivu makali ya mgongo ambayo ni changamoto kwa watu wengi.

Dk Minja amesema kutakuwa na madarasa maalum ya lishe bora ambapo wananchi watapewa elimu bure kuhusu lishe bora.

“Tunatoa wito kwa wananchi kutumia fursa hiyo adhimu kufika katika banda namba 12 la MOI kwa ajili ya kupata huduma hizo za kibingwa na tutawahudumia wote na endapo mgonjwa atahitaji rufaa atapewa moja kwa moja.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button