JMK Park, ICARRe kuibua vipaji kikapu

Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) limeingia makubaliano ya miaka miwili na taasisi ya kijamii ya Marekani ya ICARRe kwa lengo la kukuza vipaji vya mchezo huo kwa watoto na vijana.

Kwa mujibu wa taarifa ya TBF iliyotolewa na Ofisa Habari Mary Arthur,makubaliano hayo yaliyofanyika Dar es Salaam yanakusudia kushughulikia changamoto zinazokabili vituo vya mafunzo ya mpira wa kikapu vinavyosimamiwa na TBF, ikiwemo upungufu wa vifaa na hitaji la wakufunzi wa Kitaalamu.

Advertisement

SOMA: Mzumbe waandaa tamasha kuibua vipaji