Kamala Harris kutoa ripoti ya afya yake leo

Mgombea urais wa Marekani kupitia chama cha Democrat, Kamala Harris.

MGOMBEA urais wa Marekani kupitia chama cha Democrat, Kamala Harris leo anatarajiwa kutoa ripoti ya historia yake ya tiba na afya kuthibitisha kuwa yuko sawa kiafya kuwa rais.

Ofisi ya Harris mwenye umri wa miaka 59 haijafafanua zaidi kuhusu undani wa ripoti utakavyokuwa.

SOMA: Trump kagoma kutoshiriki mdahalo

Advertisement

Hata hivyo msaidizi wa Harris, ambaye amezungumza kwa sharti la kutotajwa jina kujadili suala nyeti, amesema ripoti hiyo inahitimisha kwamba Harris “ana uimara wa kimwili na kiakili unaohitajika ili kutekeleza majukumu ya urais kwa mafanikio, yakiwemo yale ya Mtendaji Mkuu, Mkuu wa Nchi na Kamanda Mkuu.”

Mgombea wa urais wa Marekani kupitia Republican, Donald Trump.

Kwa upande wake mgombea wa Republican Donald Trump ametoa taarifa fupi mno ikiwemo baada ya sikio lake kuchanwa na risasi wakati wa jaribio la kumuua Julai.

Trump mwenye umri wa miaka 78 aliwahi kuhoji afya ya Rais Joe Biden wakati kiongozi huyo wa Marekani alipokuwa akisaka kuchaguliwa tena.