Wizara ya Katiba na Sheria imewasilisha Randama ya Mpango wa Bajeti ya mafungu yaliyopo chini ya Wizara kwa mwaka 2025/2026 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala, Katiba na Sheria Bungeni jijini Dodoma.
Kikao hicho kimeongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Florentin Kyombo na kwa upande wa Wizara, Dk Damas Ndumbaro aliambatana na Uongozi wa Wizara na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara.
Majadiliano hayo ni sehemu ya utekelezaji wa shughuli za Kamati za Kudumu za Bunge zinazoendelea katika kipindi hiki ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya kuelekea katika vikao vya Bunge la Bajeti.