Karia mgombea pekee urais TFF

DAR ES SALAAM; RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ndiye mgombea pekee wa nafasi hiyo kwenye uchaguzi wa shirikisho hilo utakaofanyika Tanga, Agosti 16 mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Kiomoni Kibamba amesema mgombea huyo ndiye pekee aliyekidhi sifa kati ya wagombea wote waliojitokeza kuomba nafasi hiyo. Wagombea walioenguliwa ni Ally Mayay, Shija Richard, Dk Mshindo Msolla, Mustapha Himba na Ally Mbingo.