Kaya Elfu-11 kunufaika bima ya afya kwa wote Geita

JUMLA ya kaya 11,276 zenye wananchi wapatao 69,651 wasiomudu gharama za matibabu mkoani Geita wanatarajia kunufaika na mpango wa Bima ya Afya kwa Wote chini ya ufadhili wa serikali.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashimu Komba ameeleza hayo katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa bima ya afya kwa wote ngazi ya mkoa iliyofanyika mji mdogo wa Katoro.
Komba amesema wanufaika hao wamelipiwa gharama zote katika awamu ya kwanza ya mpango wa bima ya afya kwa wote na mpango huo ni endelevu kuhakikisha kila mtanzania anapata uhakika wa matibabu.

Aidha amewataka wakazi wa Geita kulibeba jambo hilo kwa uzito wake kwa kuzingatia kuwa hakuna mwenye taarifa za maradhi ama ugonjwa hivo ni vyema kuweka dhama ya bima ya afya kwa wote.
Komba ameagiza waganga wakuu na wafawidhi wa hospitalI zote za halmashauri chini yam ganga mkuu wa mkoa kusimamia kwa weledi uhakika wa matibabu kwa wanufaika wote wa bima ya afya kwa wote.
“Hakikisheni mnasimamia wananchi hawa wanapata huduma bila kikwazo chochote tutakapo sikia vinginevyo hatutasita kuwachukulia hatua kali” amesisitiza Komba.

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa bima ya Afya mkoa wa Geita, (NHIF) Elias Odhiambo amesema serikali imeweka imejizatiti kuhakikisha kila kaya iliyowekwa kwenye mpango huo inapata huduma ya afya bila usumbufu.
“Tunajua hii ni awamu ya kwanza ya serikali yetu kuwatambua wale wanaopatikana kwenye mpango wa kaya maskini, Lakini itakuja awamu ya pili ambayo itajumuisha watu wote”, amesema Odhiambo.
Kwa upande wake mkazi wa mamlaka yam ji mdogo wa Katoro, Christina Shija amekiri kuwa mpango huo utaokoa maisha ya wananchi wengi wa kawaida kutokana na kupanda kwa gharama za matibabu.
“Kwakweli tulikuwa tunapitia changamoto sana, kwetu sisi wazee unafika pale hospitali unaenda kupima unaambiwa tatizo ni kubwa sana leta hela hela unakuta hauna”, amesema Christina.
Naye Joshua Lazaro amesema mpango wa bima ya afya kwa wote unaenda kuwa mkombozi kwa wananchi wengi kwa kuweka uhakika wa kupata vipimo vya magonjwa, kumuona daktari na kununua dawa.




Sauti ya Mungu hata Bima ya Afya imejaa tele Afya inalindwa masaa 24 kama ATM
I just came across this amazing way to earn $6,000-$8,000 a week online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
Follow Here ……………………… https://Www.Cash54.Com
I am making a real GOOD MONEY (300$ to 400$ / hr )online from my laptop. Last month I GOT check of nearly 18,000$, this online work is simple and straightforward, don’t have to go OFFICE, Its home online job. At that point this work opportunity is for you.if you interested.simply give it a shot on the accompanying site….Simply go to the BELOW SITE and start your work…
.
More Details For Us→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com
Sauti ya Mungu hata Bima ya Afya imejaa tele Afya inalindwa masaa 24 kama ATM
Sauti ya Mungu hata Bima ya Afya imejaa tele Afya inalindwa masaa 24 kama ATM.
Sauti ya Mungu hata Bima ya Afya imejaa tele Afya inalindwa masaa 24 kama ATM.