Kazumari Mwenyekiti Kamati ya Tuzo za TASWA

DAR ES SALAAM: KAMATI ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), imemteua Jemedari Said Kazumari kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za Wanamichezo Bora Tanzania zinazotolewa na TASWA.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa TASWA, Alfred Lucas inaeleza kuwa TASWA imerejesha utoaji wa tuzo zake kama ilivyokuwa miaka ya nyuma na zitaanza tuzo za kila mwezi kuanzia Julai 2023 hadi Juni 2024, kisha itafanyika sherehe ya kuzawadia wanamichezo wote waliofanya vizuri mwaka 2023/24 kwa michezo mbalimbali kadri Kamati ya Utendaji ya TASWA itakavyopanga kwa ushauri wa Kamati ya Tuzo.

Jemedari ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari, akiwa pia na leseni B ya ukocha wa mpira wa miguu, ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu katika timu mbalimbali nchini na nje ya nchi, amepata kuwa Meneja wa Leseni za Vilabu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) na Ofisa Maendeleo wa shirikisho hilo kwa miaka minne.

Pia alikuwa Meneja wa timu ya Azam FC iliyochukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2012/2013, amepata kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF na pia Mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72). Pia ni mfuatiliaji mzuri wa michezo mbalimbali.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo atakuwa Mbonile Burton, ambaye amepata kuwa Rais wa Chama cha Gofu Wanawake Tanzania (TLGU). Pia ni mtaalam wa michezo ya tenisi, kriketi, skwashi, mpira wa meza, vinyoya na riadha.

Katibu wa kamati hiyo atakuwa Ramadhan Mbwaduke, ambaye amekuwa mwandishi wa habari za michezo kwa zaidi ya miaka 20 akiwa katika ngazi ya uhariri, pia ni mtaalamu wa michezo mbalimbali nchini.-

Wajumbe ni Tullo Chambo,Wilson Oruma, Patrick Nyembera, Evance Mhando, Amry Masare, Aaron Mpanduka, Ramadhani Mwelondo, Cosmas Mlekani, Adam Lutta, Gift Macha, Charles Abel, Paschal Kabombe, Mussa Mwakisu, Anuary Binde, Rahel Pallangyo, Tagato James, Ezekiel Mwambopo, Alex Luambano, Faustine Felician, Abisay Stephen Jr, Abdul Mkeyenge, Yusuph Badi, Omary Katanga, Irene Kilango, Athanas Kazige, Suleiman Jongo, Fatma Chikawe na Abdallah Ibrahim.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
NieveHill
NieveHill
2 months ago

I’ve gained only within four weeks by comfortably working part-time from home. Immediately when I had lost my last business, mtg I was very troubled and thankfully
following website___________ http://Www.Careers12.com

Last edited 2 months ago by NieveHill
Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x