Kenya matumaini makubwa bomba la gesi Dar-Mombasa

Kenya matumaini makubwa bomba la gesi Dar-Mombasa

KENYA inakusudia kuendelea na ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Dar es Salaam nchini Tanzania, hadi mji wake wa pwani wa Mombasa na baadaye mji mkuu Nairobi, ikiwa ni mpango wa kupunguza gharama za nishati, Rais wa Kenya William Ruto amesema.

Ripoti za ndani zinaweka gharama ya bomba la kilomita 600 kuwa takriban $1.1bn (Shilingi trilioni 2.56).

Rais Ruto ameviambia vyombo vya habari vya Tanzania, muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na Rais Samia Suluhu Hassan, katika ziara yake ya kwanza nchi Tanzania tangu aingie madarakani Septemba, kwamba mradi huo utashusha bili za umeme kwa viwanda na matumizi ya nyumbani.

Advertisement

Mapema leo akiwa mkoani Mtwara, Mkurungenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli Nchini (PURA), Mhandisi Charles Sangweni, alisema serikali ya Tanzania imeokoa kiasi cha shilingi trilioni 121, sawa na dola za Marekani bilioni 52 tangu kuanza kutumia nishati ya gesi asilia kuzalisha umeme nchini mwaka 2004.

Mhandisi Charles Sangweni amesema kwa sasa gesi asilia inachangia asilimia 70 upatikanaji wa umeme nchini.

Mhandisi Sangweni ameeleza hayo wakati wa ziara ya bodi ya Wakurungezi wa Mamlaka hiyo, wajumbe wa kamati za bodi, menejimenti ya PURA na baadhi ya wataalamu wa mamlaka hiyo waliotembelea eneo uchimbaji wa gesi asilia,  Ntorya, mkoani Mtwara.

Amesema kabla ya kuanza kutumia gesi, uzalishaji wa umeme nchini uliigharimu serikali fedha nyingi kununua nishati ya mtafuta.

Amesema iwapo serikali itaendelea kuwekeza zaidi kwenye miundombinu ya usafirishaji wa gesi, itawezesha nishati hiyo kufika na kutumika maeneo mengi na kuendelea kuokoa fedha nyingi, ambazo zitatumika kwenye matumizi mengine kwa manufaa ya taifa.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *