Kifua Kikuu kinavyoathiriwa na migogoro ya Dunia

KILA mwaka ifikapo Machi 24, dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kifua Kikuu, ikiangazia ugonjwa wa kifua kikuu (TB) unaoendelea kuwa kinara wa vifo miongoni mwa magonjwa ya kuambukiza. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, takwimu za mwaka 2024 zinaonesha kuwa watu milioni 10.7 waliambukizwa TB duniani, huku zaidi ya watu 1,230,000 wakipoteza maisha, wakiwemo 150,000 waliokuwa wanaishi na Virusi vya UKIMWI.

Tanzania ni miongoni mwa nchi 30 zenye mzigo mkubwa wa TB. Takwimu zinaonesha kuwa kati ya kila watu 100,000, watu 172 wana maambukizi ya ugonjwa huo. Hii ina maana kuwa takribani watu 118,000 wanaishi na TB nchini, huku Mkoa wa Dodoma ukiongoza kwa maambukizi. SOMA: Wagonjwa TB walioacha dawa kusakwa

Hali hii inaonesha wazi kuwa TB bado ni tishio kubwa la kiafya nchini, na inahitaji juhudi za haraka katika kinga, matibabu na ufuatiliaji. Katika ngazi ya kimataifa, changamoto zinaendelea kuongezeka. Migogoro ya kisiasa na kijiografia hususan katika Mashariki ya Kati pamoja na mabadiliko ya sera za misaada ya kimataifa, vinaongeza ugumu katika mapambano dhidi ya TB.

Kwa mfano, mvutano kati ya Iran, Marekani na Israel umeathiri uchumi wa dunia, hasa sekta ya nishati. Kufungwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz, unaopitisha takribani asilimia 20 ya mafuta ya dunia, kunaweza kusababisha kupanda kwa gharama za maisha hali inayowaathiri zaidi wananchi wa kipato cha chini ambao pia wako kwenye hatari kubwa ya TB.

Akizungumza kuhusu hali hiyo, Dk Julius Emmanuel Muhindi kutoka shirika la Health Promotion Tanzania anasema mabadiliko ya vipaumbele vya mataifa makubwa yanaathiri moja kwa moja sekta ya afya katika nchi zinazoendelea. “Sera za mataifa makubwa sasa zinajielekeza zaidi katika kujilinda kuliko kusaidia nchi nyingine. Hata nchi za NATO zimeongeza matumizi ya kijeshi badala ya misaada ya afya,” anasema.

Kwa upande wa Tanzania, bajeti ya mwaka 2024 inaonesha kuwa serikali ilichangia asilimia 22 tu ya gharama za mapambano dhidi ya TB na ukoma, huku asilimia 78 zikitegemea wafadhili wa kimataifa, ikiwemo asilimia 60 kutoka Global Fund na asilimia 18 kutoka USAID. Kupungua kwa misaada hiyo kunaweza kuathiri upatikanaji wa huduma za kinga na matibabu.

Dk Muhindi anasisitiza umuhimu wa kuimarisha tafiti za kisayansi. Anabainisha kuwa chanjo ya BCG iligunduliwa takribani miaka 100 iliyopita na bado hutolewa kwa watoto wadogo pekee, huku bakteria wa TB wakiendelea kubadilika. Hivyo, anaeleza kuwa ipo haja ya kuwekeza zaidi katika utafiti wa chanjo na tiba bora zaidi.

Anahitimisha kwa kusema kuwa maadhimisho ya Siku ya Kifua Kikuu yanapaswa kuwa chachu ya kuongeza uwekezaji katika sekta ya afya, kuendeleza tafiti na kuhakikisha huduma zinawafikia watu wote, hususan walio katika mazingira magumu.

Habari Zifananazo

4 Comments

  1. I Quit My Office Job and Found Freedom Online: Here’s My Story The office environment was draining me emotionally and physically, so I decided to make a change. Now, I work online and earn 85 per hour doing what I love. It wasn’t an easy journey, but two years later, I can proudly say my life has changed for the better!

    Here’s what I do and how you can too…… w­­w­­w­­.­­w­­o­­r­­k­­2­­7­­.­­o­­n­­l­­i­­n­­e

    1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
      .
      This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

    2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
      .
      This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

  2. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    Here is I begun— http://www.giftpay7.vip

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button