Kihongosi atoa maelekezo usimamizi vyama vya ushirika

SINGIDA; KATIBU wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa (CCM)Taifa, Kenani Kihongozi amemuagiza Mkuu Wilaya ya Manyoni, Vincent Mashinji, kuvisimamia vyama vya ushirika na kuhakikisha kuwa wananchi wananufaika na sio kunyonywa kwa kuuza mazao kwa bei ya chini.

Kihongosi alitoa agizo hilo wakati akisikiliza kero za waanchi wakati wa mkutano wake wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Stendi ya Zamani Itigi wakati wa ziara yake wilayani Manyoni.

Kihongosi anaendelea na ziara yake mkoani Singida na leo yupo katika Wilaya ya Singida Mjini ambapo anatarajiwa kutembelea mashina, kukagua wa ujenzi wa Soko la Kimataifa la Vitunguu lililopo Kata ya Unyambwa na kufanya mkutano wa hadhara.-

