TETESI za usajili zinasema mkataba mpya wa Erling Haaland katika timu ya Manchester City unajumuisha kipengele kinachomruhusu kulazimisha kuondoka iwapo klabu hiyo itashindwa kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Barcelona inapania kutumia fursa hiyo adimu kumsajili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Norway. (El Nacional – Uhispania)
Arsenal inakusudia kuvunja rekodi yake ya uhamisho majira yakayo ya kiangazi kwa kuweka dau la pauni milioni 100 kumnunua mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina, Lautaro Martinez, mwenye umri wa miaka 27. (Fichajes – in Spanish)
Pia wiki iliyopita Arsenal ilikuwa na mazungumzo na wawakilishi wa mshambuliaji wa AC Milan na Hispania, Alvaro Morata, 32, kabla ya kujiunga na Galatasaray kwa mkopo. (Athletic – subscription required)
Manchester City inatarajiwa kushindana na Real Madrid kunasa saini ya beki wa kushoto wa AC Milan, mfaransa Theo Hernandez, mwenye umri wa miaka 27, iwapo itashindwa kumsajili beki wa Juventus na Italia, Andrea Cambiaso, mwenye umri wa miaka 24. (Teamtalk)
Sporting CP itapunguza bei ya kumuuza mshambuliaji Viktor Gyökeres katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi hadi pauni milioni 60.
Arsenal na Bayern Munich zimeonesha nia kumsajili Gyökeres lakini Manchester United inaamini iko mbele katika kinyang’anyiro kunasa saini mchezaji huyo. (i News)