DAR-ES-SALAAM: Shirika la AHEAD limeahidi kuendelea kutoa msaada kwa Tanzania katika utoaji wa huduma muhimu kama afya, kilimo na elimu, lengo likiwa kuboresha maisha ya watu.
Akifungua kongamano la “Ubora wa Huduma za Afya 2024” jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Shirika hilo, Dk. Donna Williams, amesisitiza azma ya shirika lake kuendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha huduma hizo zinawafikia wengi, hasa wale wenye uhaba wa rasilimali, na zinakuwa endelevu.
“sisi kama watoto wa waanzilishi wa Shirika la AHEAD litahakikisha programu hizi za huduma zinawafikia wengi wenye uhaba wa rasilimali na zinakuwa endelevu,” amesema Dk. Williams.
Kongamano hilo la kihistoria lilowakutanisha wadau wa afya linalenga kuwa chachu ya mabadiliko chanya kwenye sekta hiyo muhimu nchini Tanzania, kwa kusisitiza umuhimu wa huduma bora za afya zinazotolewa na watu wa ndani.
“Kongamano linalenga kuwa chachu ya mabadiliko katika sekta ya afya nchini likisisitiza umuhimu wa kutoa huduma bora za afya kwa watanzania kwa kutumia watu wetu,” alisema Mkurugenzi.
SOMA : https://habarileo.co.tz/ummy-awaita-wadau-sekta-ya-afya/