DAR ES SALAAM: NAIBU Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP) Mkondya leo, Machi 18, 2025, ameongoza waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi Chanika, Dar es Salaam, SP Awadh Mohamed Chico, ambaye alifariki jana katika ajali ya gari akiwa anaelekea kazini.
Naibu Kamishina Mkondya alitoa salamu za rambirambi kwa familia ya marehemu kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Camillus Wambura.
“Safari ya umauti ni ya kila mmoja wetu,” amesema huku akiiomba jamii kuwa wavumilivu na kuendelea kumuombea marehemu.