Maafisa ugani washauriwa kutoa utalaamu kilimo

MKUU wa wilaya ya Monduli, Festo Kiswaga amewataka maofisa ugani kutoa ushauri wa kitaalamu utakaowawezesha wananchi kupata mazao mengi katika kilimo kwa lengo la kusaidia kujiongezea kipato.

Kiswaga amesema wakati wa kuwakabidhi vishikwambi 35 na magwanda maofisa ugani hao katika hafla fupi iliyofanyika ofisi ya halmashauri ya wilaya hiyo.

SOMA: Maofisa ugani wapikwa mfumo wa CSDS

Kiswaga amesema ili uchumi wa wilaya hiyo uweze kukua zaidi inahitaji wananchi waongeze fursa nyingine ya kilimo badala ya kutegemea mifugo pekee.

Amesema kupitia maofisa hao anaamini wananchi watapata utaalamu utakaowawezesha kulima kisasa ili kuzalisha zaidi.

Habari Zifananazo

Back to top button