Maboresho yanakuja elimu

DAR ES SALAAM: SEKTA ya elimu inatarajia kufanya maboresho makubwa baada ya serikali kwa kushirikiana na wadau kuanza tathmini ya maeneo ya vipaumbele yatakayoboresha sekta hiyo.

Maboresho hayo yanalenga uendelezaji wa taaluma ya ualimu, mpangilio mzuri wa ajira za wanataaluma hao utakaolingana na mahitaji yao.

Hatua hiyo ni badaa ya serikali kutimiza vigezo ili kunufaika na mradi wa Dola 167 milioni ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 454.04, zinazotolewa na Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE), ambapo kwa sasa ipo katika tathmini kwa ushirikiano na wadau.

SOMA: TET yawasilisha mabadiliko ya mitaala mipya ya elimu

Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Atupele Mwambene ametoa taarifa hiyo katika kikao cha wadau katika mapitio ya tathmini ya mradi huo.

Meneja Programu Mwandamizi wa GPE kutoka Ubalozi wa Sweden, Stella Mayenje amesema kupitia mradi huo Tanzania ilinufaika awali kwa kupata Dola milioni 84 ambazo ni sawa na zaidi ya Sh bilioni 228.3.

SOMA: Serikali yaita wadau kushirikiana katika elimu

Mayenje amesema Tanzania imepata kiasi hicho anachoeleza kwamba ni kidogo ni kutokana na kutotimiza baadhi ya masharti ambayo kwa sasa yanafanyiwa kazi ili kuyatimiza.

Habari Zifananazo

Back to top button