MWENYEKITI wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika yasiyo ya kiserikali nchini (NACONGO) Mwantumu Mahiza ameyanyooshea kidole baadhi ya mashirika yanayofanya kazi zake mkoani Kigoma akisema yapo yasioyo na tija kwa jamii zaidi ya kujitpatia fedha zinazopatikana kwenye mashirika hayo kunufaisha watendaji wa mashirika hayo.
Mahiza amesema hayo wakati akifungua mkutano wa mashirika yasiyo ya serikali mkoani humo na kusema kuwa baadhi ya mashirika yamefanya kazi nzuri na kuleta tija kwa wananchi na kimkoa kwa jumla lakini baadhi yamekuwa yakitumiwa na viongozi wake kwa ajili ya manufaa yao binafsi.
Sambamba na hilo Mahiza amesema baadhi ya mashirika hayo hutumia fursa za kuwapiga picha wananchi masikini na mazingira yao kisha kwenda kuombea fedha kwa wahisani na ambaoo fedha hizo hazipelekwi kwa wananchi hao bali viongozi viongozi hao kujinufaisha wenyewe na kwamba jambo hilo halikubaliki.

Akifungua mkutano huo Mkuu wa Mkoa Kigoma, Thobias Andengenye ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotekeleza majukumu kupitia miradi mbalimbali mkoani humo kujikita maeneo ya vijijini na kutoa huduma zenye kubeba vipaumbele vya wananchi.
Amesema pamoja na mchango mkubwa wa mashirika hayo uliofikia Shilingi bilioni 24 kwa mwaka 2023, kwa ajili ya kuwezesha miradi ya kutolea huduma kwa jamii, bado baadhi yao yameshimdwa kuwasilisha taarifa za utendaji kazi wao kwa mamlaka zinazosimamia uratibu wa kazi zao hali inayotilia shaka utendaji kazi wao kwenye shughuli za wananchi.

Awali mjumbe wa NACONGO Taifa kutoka mkoa wa Kigoma, Alex Luoga amesema mashirika mengi ya kiserikali mkoani humo hayana bajeti za moja kwa moja za kutekeleza shughuli zao kama zilizvyoainishwa kwenye usajili wao tofauti na mashirika ya kimataifa hivyo kumekuwa na mtazamo tofauti na kuonekana kama wababaishaji wasiofanya kazi.