‘Majogoo’ kung’ang’ania kileleni EPL leo?

MICHEZO ya soka ya Ligi tano bora barani Ulaya inaendelea leo kwa mitanange kadhaa kwenye viwanja tofauti.

Katika Ligi Kuu England(EPL), majogoo wa jiji la Liverpool inaongoza ligi ikiwa na pointi 25 baada ya michezo 10 wakati huko Hispania miamba ya kikatalunya, Barcelona inaongoza LaLiga ikikusanya pointi 33 katika michezo 12.

Wenyeji wa Bavaria huko Ujerumani, Bayern Munich ipo juu ya msimamo wa Bundesliga ikiwa na pointi 23 baada ya michezo tisa wakati magwiji wa jiji la Naples nchini Italia, Napoli inaongoza Serie A ikiwa na pointi 25 baada ya michezo 11.

Advertisement

SOMA: Real Madrid vs Barcelona: ‘El Clásico’ ya kibabe

Bingwa mtetezi wa Ligue 1 huko Ufaransa Paris Saint-Germain bado inaendelea kuongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 25 baada ya michezo 10.

Zifuatazo ni mechi za ligi hizo leo:

PREMIER LEAGUE:
Brentford vs Bournemouth
Crystal Palace vs Fulham
West Ham United vs Everton
Wolves vs Southampton
Brighton vs Manchester City
Liverpool vs Aston Villa

LALIGA
Real Madrid vs Osasuna
Villarreal vs Deportivo Alaves
Leganes vs Sevilla

BUNDESLIGA
Mainz 05 vs Borussia Dortmund
St. Paul vs Bayern Munich
VfL Bochum vs Bayer Leverkusen
Werder Bremen vs Holstein Kiel
RB Leipzig vs Borussia M’gladbach

SERIE A
Venezia vs Parma
Cagliari vs AC Milan
Juventus vs Torino