MACHO na masikio ya wapenda soka duniani leo yanahamia Hispania ambako kunapigwa kipute kikali cha ‘El Clásico’ Ligi Kuu Hispania-LaLiga kati ya miamba Real Madrid na Barcelona.
Real Madrid ni bingwa mtetezi wa taji la ligi hiyo wakati Barcelona ndio vinara katika msimamo kwa sasa ikiwa na pointi 27 ikifuatiwa na Real yenye pointi 24.
SOMA: Laliga kuanza kutimua vumbi leo
Mtanange huo unapigwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu wenye uwezo wa kuingiza watazamaji 78,297 uliopo mji mkuu wa Hispania, Madrid.
Real Madrid inaongoza kwa kushinda El Clásico ikishinda mara 105 wakati Barcelona ina 100 huku zikitoka sare mara 52.
Katika kambi ya Barca kocha wa Kijerumani Hansi Flick amefanya mapinduzi mkubwa kwa kuimarisha wachezaji kama Marc Casadó, Pedri, Raphinha, Lamine Yamal, na Robert Lewandowski ikilinganishwa na mwanzoni mwa msimu, kwani kwa hatua ndogo ndogo imekuwa ikiboresha mchezo wao na, zaidi ya yote, ufanisi wao kwa point.
Nako Real Madrid wachezaji kama Federico Valverde na Jude Bellingham wamekuwa na kiango bora katika nafasi zao, huku Vinícius Júnior na Kylian Mbappé wakiongoza safu ya ushambuliaji.
Mechi nyingine za LaLiga leo pamoja na ligi nyingine nne bora Ulaya leo ni kama ifuatavyo:
PREMIER LEAGUE
Aston Villa vs Bournemouth
Brentford vs Ipswich Town
Brighton vs Wolves
Manchester City vs Southampton
Everton vs Fulham
LALIGA
Real Valladolid vs Villarreal
Rayo Vallecano vs Deportivo Alaves
Las Palmas vs Girona
BUNDESLIGA
Augsburg vs Borussia Dortmund
RB Leipzig vs Freiburg
St. Paul vs Wolfburg
VfB Stuttgart vs Holstein Kiel
Werder Bremen vs Bayer Leverkusen
SERIE A
Napoli vs Lecce
Bologna vs AC Milan
Atalanta vs Hellas Verona
LIGUE 1
Angers vs Saint-Etienne
Reims vs Brest
Lens vs Lille