Makala 172 TSN zapaisha utalii

DAR ES SALAAM: Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) imeendelea kutekeleza maono ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan, kwa kuimarisha jitihada za kuitangaza sekta ya utalii kupitia uandishi na uchapishaji wa makala maalumu.

Katika kipindi husika, TSN imeandaa jumla ya makala 172 zilizolenga kuibua na kuonesha vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini, sambamba na kuangazia mafanikio ya sekta hiyo katika kuchangia ukuaji wa uchumi.

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo. Paul Makonda ameeleza hayo leo Mei 4, 2026 bungeni wakati akiwasilisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2026/27.

Makala hizo pia zimeelekeza nguvu katika kuonesha fursa za ajira na uwekezaji zinazopatikana kupitia utalii, pamoja na mchango wake katika kukuza pato la Taifa na ustawi wa wananchi kwa ujumla.

Kwa mujibu wa mpango wa kimkakati wa kampuni hiyo, maudhui hayo yamelenga kuitangaza Tanzania kimataifa kama moja ya vivutio bora vya utalii na uwekezaji, huku yakisaidia kuongeza uelewa wa umma kuhusu umuhimu wa sekta hiyo katika maendeleo ya nchi.

Hatua hiyo inaonesha dhamira ya TSN ya kutumia vyombo vya habari kama jukwaa muhimu la kukuza sekta ya utalii na kuunga mkono juhudi za Serikali za kuvutia watalii na wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button