Makalla akemea imani za kishirikina

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa(CCM-NEC),Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla amewataka wananchi wa Wilaya ya Kiteto na Watanzania kwa ujumla kuacha imani za kishirikina katika jamii zao.

Makalla ameyasema hayo leo Septemba 9, alipozungumza na wananchi wa Engusero, Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake Arusha na Manyara.

SOMA: CCM hatubebwi tumejipanga- Makalla

Makalla ametoa pole kwa matukio maovu ya ulawiti yanayoendelea katika jamii na kuwataka wanamume kwa wanawake katika jamii kukemea vikali na kuachana na mambo ya ushirikina ambayo yanapelekea wao kufanya matukio hayo.

“Nitoe pole kwa matukio yanayoendelea kutokea ya ulawiti nimepewa taarifa kuwa kuna mama na mtoto huko Dodoma ambao ni wakazi wa kiteto wamefanyiwa vitendo vibaya,” amesema Makalla.

SOMA: CCM yatoa kauli kifo kada wa Chadema

Ametoa wito kwa viongozi wa dini na kimila kukemea matukio hayo kwani waganga wanaowashinikiza kufanya vitendo hivyo ni waongo.

Habari Zifananazo

Back to top button