Makonda aonya viongozi wa michezo wasiowajibika

DAR ES SALAAM: WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amewaonya viongozi wa mashirikisho ya michezo nchini wanaoshindwa kutekeleza ahadi walizozitoa kwa wanachama wao kuwa wako hatarini kung’olewa madarakani.

Makonda amesema ofisi yake itaanza kufuatilia utekelezaji wa ahadi hizo na endapo itabainika kuwa hazijafikia hata asilimia 20 ya yale waliyoahidi wakati wa uchaguzi, wizara itashirikiana na wanachama kuleta mabadiliko ya uongozi.

Akizungumza Dar es Salaam leo katika mkutano wa viongozi hao na Baraza la Michezo la Taifa (BMT), uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Makonda amesema viongozi wengi waliingia madarakani kwa ahadi nyingi lakini utekelezaji wake ni mdogo.

“Nyinyi mlipata nafasi hizi kwa kupigiwa kura na wanachama wenu. Ni lazima mujiulize mmetimiza kwa kiwango gani ahadi mlizotoa kwa waliowachagua,” amesema.

Amesema kuwa serikali haitaridhika kuona viongozi wanaendelea kushikilia madaraka bila kuonesha matokeo katika maendeleo ya michezo.

Amesema amepewa jukumu la kuhakikisha sekta ya michezo inaleta matokeo kwa taifa, hivyo viongozi wa mashirikisho wanapaswa kuwajibika kwa wanachama na kwa maendeleo ya michezo nchini.

Amewataka viongozi hao kuimarisha uwazi katika uendeshaji wa mashirikisho yao na kushughulikia migogoro ya ndani inayokwamisha maendeleo ya michezo.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
    .
    This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com

    1. Many people in the United States and other parts of the world have lost their regular occupations. This was terrible, and I understand how you felt when you had no money left for your family. But I’m here to give a simple method that will fix all of your money issues right now. Working from home might earn you more than $15k each month simply by remaining at home. So, for further information, go to this website immediately and start earning right away………..

      GOOD LUCK. ==-…………………………….-=>>) https://earnsmartwithus.netlify.app/

  2. I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
    .
    This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button