“Mamlaka inachangia ongezeko la chakula”

DODOMA: MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu nchini, (TPHPA), Profesa Joseph Ndunguru amesema mamlaka hiyo ina mchango mkubwa katika kutosheleza chakula hasa kutokana na jitihada za kudhibiti visumbufu vya mazao.

Profesa Ndunguru amesema hayo Agosti 19, 2024 katika maonesho ya wakulima, wafugaji na vavuvi yaliyomalizika hivi karibuni.

Amesema katika siku za karibuni mamlaka hiyo ilifanikiwa kudhibiti ndege aina ya kwelea kwelea ambao walikuwa wakishambulia mashamba makubwa ya mpunga.

SOMA: Sh bilioni 2 kuboresha huduma ukaguzi TPHPA

“Tunaona mamlaka ikidhibiti tija ikaongezeka inachangia kwenye ongezeko la chakula, pia inaimarisha masoko,” amesema.

SOMA: Rais Samia ateua bosi TPHPA

Akimnukuu Rais Samia Suluhu Hassan aliyesema Tanzania ina utoshelevu wa chakula, amesema mamlaka ina mchango mkubwa katika hilo kwa kuwa inadhibiti visumbufu mbalimbali vya mazao wakiwepo ndege hao wa kwelea kwelea, panzi, panya na viwavi jeshi vamizi.

Habari Zifananazo

Back to top button