TETESI za usajili zinasema Manchester United imeonesha nia kumsajili kiungo mshambuliaji wa Roma, Paulo Dybala majira yajayo ya kiangazi ambapo atakuwa amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake. (Fichajes – Spain)
Liverpool itarejea kwa beki wa kati wa Nottingham Forest anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 80 Murillo Santiago Costa dos Santos maarufu Murillo iwapo Virgil van Dijk hataongeza mkataba wake Anfield.
Beki huyo raia wa Brazil anapenda kujiunga na Liverpool licha ya kusaini mkataba mpya Forest hivi karibuni. (CaughtOffside)
Kipau mbele kikuu cha Arsenal dirisha la usajili majira yajayo ya kiangazi kinabaki kuwa fowadi wa Athletic Club, Nico Williams. (Football Transfers)
Uthamini wa Chelsea wa Christopher Nkunku ulizuia uhamisho katika muda wa mwisho kwenda Bayern Munich au Man Utd. (Mail Sport)
Fermín López hajafuta uwezekano wa kuondoka Barcelona majira yajayo ya kiangazi licha ya kukataa ofa za Manchester United na Juventus.
Hatahivyo, Chipukizi huyo wa kihispania anapenda kujiunga na Bayern Munich. (El Nacional – Spain)