TETESI za usajili zinasema Manchester United imetoa ofa kwa Jadon Sancho kumpeleka Atletico Madrid, Napoli na PSG ili asajiliwe. Winga huyo pia anatambua kwamba Juventus inafikiria uhamisho wake. (CaughtOffside)
Uongozi wa Manchester United umeripotiwa kuwa unajaribu kupima nia kutoka kwa klabu hizo, wakitumaini kupata mahali pazuri kwa winga huyu ambapo anaweza kuendeleza taaluma yake.
Sancho alijiunga na Manchester United wakati wa majira ya kiangazi ya 2021 kutoka Borussia Dortmund katika uhamisho uliosubiriwa kwa hamu kubwa.
Soma zaidi: Sancho ajiunga Dortmund
Uhamisho huu ulionekana kama biashara muhimu kwa United, ambayo ilikuwa ikimfukuzia kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Muda wa Jadon Sancho akiwa Manchester United umejaa kupanda na kushuka.
Licha ya kuonyesha umahiri, hajapata nafasi ya mara kwa mara katika kikosi cha kwanza.
Mabadiliko ya kocha Old Trafford pia yameathiri mwenendo wa Sancho baada ya kutokuwa na maelewano mazuri kati yao.
Katika miezi ya hivi karibuni, uvumi kuhusu mustakabali wa Sancho Manchester United umeongezeka.
Ripoti zinaonyesha kuwa klabu iko tayari kumuuza winga huyo ili kutoa nafasi kwa wachezaji wapya na kurejesha sehemu ya uwekezaji uliowekwa kwake.
Kadri dirisha la uhamisho linavyoendelea, itakuwa ya ni jambo la kuvutia kuona jinsi sakata hilo litakavyoendelea na wapi nyota huyo inaelekea.
Katika tetesi nyingine iwapo Arsenal itaamua kumsajili fowadi mpya majira haya ya kiangazi, Mikel Arteta angependa Nico Williams wa Athletic Club kutua Emirates.(The Athletic)
Chelsea haina mpango wa kuhuisha kipengele cha kuachiwa cha pauni milioni 50 katika mkataba wa nyota wa RB Leipzig na timu ya taifa ya Hispania Dani Olmo, licha kuwepo madai ya mpango huo. (Sky Sports)
Barcelona inakabiliwa na ushindani kutoka ligi ya kulipwa Saudi Arabia kumsajili beki wa Manchester City, Joao Cancelo, huku Al Ahli na Al Ettifaq zikipima hatua hiyo. (SPORT – Spain)
Liverpool imewasilisha ombi linafikia pauni milioni 50 kumsajili beki wa kati wa Juventus, Gleison Bremer, lakini klabu hiyo ya Italia ina matumaini kumuuza kwa ada inayokaribia pauni milioni 60. (Tutto Juve – Italy)
Man Utd itawasilisha ombi la tatu kwa ajili ya kumsajili Jarrad Branthwaite wa Everton huku mashetani hao wekundu wakikusudia kumlipa mshahara wa pauni 160,000 kwa wiki. (The Times)
Kwa upande wa wachezaji wapya Man Utd ina matumaini kumsajili Manuel Ugarte kutoka PSG kwa zaidi ya pauni milioni 45. (GiveMeSport)