Marekebisho mfumo wa kodi kuipa serikali Sh tril.4

DODOMA; SERIKALI imesema mapendekezo ya kurekebisha mfumo wa kodi kwa mwaka 2025/26 yanatarajiwa kuiongezea Serikali jumla ya shilingi trilioni 4.2.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha, Dk Mwiguku Nchemba, wakati anawasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2025/26 bungeni leo Juni 12, 2025/.
“Mapendekezo ya kurekebisha mfumo wa kodi kwa mwaka 2025/26 yanatarajiwa kuiongezea Serikali jumla ya shilingi milioni 4,260,023.7,”amesema Waziri Nchemba na kutaja mapendekezo ya sheria mbalimbali yanayopendekezwa kurekesbishwa.