Mavunde aagiza mradi wa Kabanga Nickel kutekelezwa kwa wakati

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde.
SERIKALI kupitia Wizara ya Madini imeiagiza Kampuni ya ya uchimbaji wa Madini ya Tembo Nickel Corporation LTD kuhakikisha inatekeleza kwa wakati mradi wa Kabanga Nickel ambao unalenga uchimbaji wa Madini ya Nikeli na usafishaji wa madini hayo hapa nchini.
Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ametoa maagizo hayo jijini Dodoma wakati wa wasilisho kuhusu maendeleo ya mradi wa Kabanga Nikeli lililowasilishwa na Kampuni ya Tembo Nickel Corporation ambapo amesisitiza mradi huo kutekelezwa kwa wakati ili kuchochea maendeleo ya Sekta ya Madini nchini.
“Mradi huu ni mradi mkubwa na muhimu sana kwa maendeleo ya Sekta ya Madini. Tutahakikisha masuala yote yaliyobaki yanakamilika kupitia timu ya majadiliano ya Serikali na mwekezaji. Kwa upande wa mwekezaji ni muhimu kuhakikisha anakamilisha masuala yote yaliyo upande wake ili shughuli za uendelezaji wa mradi wa mgodi zianze kwa uharaka,” amesema Mavunde.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Life Zone Metals Chris Showalter amesisitiza kuhusu dhamira ya kampuni hiyo kutekeleza uendelezaji wa mradi huo utakaohusisha shughuli za uchimbaji nikeli Wilayani Ngara, Mkoa wa Kagera na ujenzi wa kiwanda cha kusafisha madini hayo kitakachojengwa Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga.
1 comments
  1. I was BROKE and desperate… now I make $3,000+ weekly from my couch! Just 30 days ago, I was stuck in a dead-end job, living paycheck to paycheck. Then I found this secret method—and everything changed Anyone can do this in their free time. Spots are LIMITED! Don’t miss out!

    Join now➤➤ http://Www.WorksProfit7.Com

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *