Mrembo Rwanda anaswa kuendesha gari amelewa

Mrembo wa Rwanda, Divine Muheto.

MSHINDI wa taji la urembo Rwanda mwaka 2022, Divine Muheto, amekamatwa kwa kosa la kuendesha gari akiwa amelewa na bila leseni.

Polisi wa Taifa wa Rwanda wamesema Muheto ameharibu miundombinu na kukimbia eneo la tukio.

Taarifa ya polisi haijaeleza iwapo mtu yeyote amejeruhiwa katika tukio hilo.

Advertisement

SOMA: Tanzania, Rwanda kukuza biashara

Kwa mujibu wa polisi hiyo si mara kwanza kwa mrembo huyo mwenye umri wa miaka 21 kuendesha gari akiwa amelewa.

Msemaji wa Idara ya Mashitaka ya Mahakama katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali amesema kesi dhidi ya Muheto itaanza kusikilizwa Oktoba 31.

Adhabu kwa mtu anayeendesha gari akiwa amelewa Rwanda ni pauni 85 na kushikiliwa polisi kwa siku tano.

 

Imetafsiriwa kutoka BBC