Miundombinu ya Usafiri Yapewa Sifa Bungeni

DODOMA: WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamesema Serikali ya awamu ya sita imefanya maboresho makubwa katika sekta ya usafirishaji, hususan katika miundombinu ya reli, anga, barabara na usafiri wa baharini.
Pongezi hizo zilitolewa wakati wa mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2025/2026, iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma, ambapo wizara hiyo imeomba kuidhinishiwa zaidi ya Shilingi trilioni 2.746.
Wakichangia bajeti hiyo, baadhi ya wabunge walisema kuwa mageuzi makubwa yaliyofanyika kwenye sekta ya usafirishaji yameongeza ufanisi wa huduma, kurahisisha safari kwa wananchi na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa.
“Tunampongeza Mheshimiwa Rais na Serikali kwa kazi kubwa inayoonekana kwenye reli, anga, barabara na hata usafiri wa baharini. Hili ni jambo la kujivunia,” alisema mmoja wa wabunge wakati wa mjadala huo.
Wabunge walisisitiza kuwa ni muhimu kuendelea kuwekeza kwenye miradi ya usafirishaji kwa kuwa ndiyo chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa Watanzania.
SOMA: Wabunge wahimiza uandaaji wa sera jumuishi za akili mnemba