Mjasiriamali Mr_Kuku afunguka gharama za bidhaa
MJASIRIAMALI Ramadhani Mwinjuma maarufu kwa jina la Mr_kuku ameiomba serikali kuangalia namna ya kupunguza gharama za vyakula ili kuendana na hali halisi ya ukubwa wa mitaji ya wafanyabiashara.
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu mapema hii leo, Mr_kuku amesema bidhaa nyingi sokoni zimekuwa bei juu hali inayotishia kukuwa kwa biashara zao.
Amesema imekuwa tofauti na miaka kadhaa nyuma ambapo licha ya gharama za maisha kuwa juu ila walau bei za bidhaa zilikuwa rafiki kwa kiasi fulani.
“Bidhaa ziko juu sana, nadhani serikali ingeangalia upande huo watuokoea sisi wajasiriamali angalau basi tuweze kujiendesha lakini kwa hali ilivyo sasa wengine wanafunga biashara zao kutokana na bidhaa kuwa juu na kama mtu ana mtaji mdogo ndo anaumia zaidi,” amesema MrKuku.
SOMA: Utafiti: Asilimia 70 biashara mpya zinakufa
Mr_kuku ambaye ni mfanyabiashara wa chakula, biriani, pilau, na kuku amesema kama gharama za bidhaa zitaendelea kuwa kubwa kwa kiwango kilichopo sasa itahatarisha ukuaji wa biashara zao.
“Kwasasa tunadumu kutokana na uzoefu tu ila mambo yakiwa hivi kuna hatari ya kukua kwa biashara zetu maana wakati mwingine hadi unaogopa kuwekeza zaidi hasa kutokana na asili ya biashara zetu,” ameongeza.
Akizungumzia ukubwa wa biashara yake, Mrkuku amesema kwa sasa anaendelea kujiwekeza zaidi na kuangalia namna anavyoweza kukua zaidi kwenye biashara yake.
SOMA: Wajasiriamali kushindanisha bidhaa zao Arusha
Pia amewashauri wale wanahitaji kuingia kwenye biashara hiyo kutokuwa na uoga kwani mwanzo huwa ni mgumu lakini baadaye biashara ikisimama kunakuwa na afadhali kulingana na wingi wa wateja.