Mkutano Mifumo ya Chakula Afrika kufanyika Dar

WIZARA ya kilimo inajipanga kushiriki Kilele cha Mkutano wa Mifumo ya Chakula Afrika 2023, utakaofanyika Septemba 5-8, 2023 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe ameeleza hayo leo Jumatatu Mei 8, 2023 wakati akiwasilisha hotuba ya makaridio ya bajeti ya wizara katika mwaka wa fedha 2023/2024.
Amesema wizara kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya kilimo nchini, itaendelea na maandalizi ya mkutano huo utakaofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Dar es Salaam.
Waziri Bashe amesema mkutano huo umelenga kuleta matokeo muhimu katika kuendeleza mifumo ya chakula na kilimo nchini na barani Afrika.
Amesema matokeo yanayotarajiwa ni pamoja na kuongezeka kwa uwekezaji katika sekta ya kilimo nchini, kukuza utalii, kuimarika kwa biashara ya mazao ya kilimo na teknolojia.