Mkutano wa majaji SEACJF fursa ya kuimarisha ushirikiano

ZANZIBAR : RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Majaji Wakuu wa Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (SEACJF) utakaofanyika Zanzibar mwakani ni fursa muhimu kuimarisha ushirikiano na utendaji wa mahakama.
Akizungumza na jopo la Majaji Wakuu waliomtembelea Ikulu Zanzibar, Dk. Mwinyi alisema mkutano huo utasaidia kubadilishana uzoefu na kujadili changamoto za kiutendaji baina ya nchi wanachama.
Dk. Mwinyi aliahidi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha mkutano huo wa kwanza unaofanyika nchini unafanikiwa.
Aliwasisitiza majaji hao kutumia fursa ya mkutano huo kutembelea vivutio vya utalii vya Zanzibar na kuwa mabalozi wa kuitangaza Zanzibar ili kuchochea sekta ya utalii inayochangia asilimia 30 ya pato la Taifa.
Kwa upande wake, Rais wa SEACJF, Jaji Mkuu wa Eswatini Moses Cuthbert Maphalala, alisema mkutano huo utalenga kuimarisha utawala wa sheria, uhuru wa mahakama na kubadilishana uzoefu ili kuhakikisha mihimili ya dola inafanya kazi kwa ushirikiano.
Hi! I could have sworn I’ve been to this blog before but after browsing through some
of the post I realized it’s new to me. Anyways, I’m definitely happy I found it and I’ll bbe book-marking and checking back frequently!