Mobetto, Aziz Ki rasmi mke na mume

DAR ES SALAAM; RASMI mwanamitindo Hamisa Mobetto ni mke wa Stephane Aziz Ki ambaye ni kiungo mshambuliaji wa Yanga baada ya ndoa yao kufungwa msikiti wa Mbweni, Dar es Salaam jana.

Aziz Ki akiwa na ndugu na wageni waalikwa walikwenda msikitini kufunga ndoa na baadaye kuelekea nyumbani kwa Hamisa kumchukua mke wake.

Ndoa hiyo ilifungishwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam, Shehe Walid Alhad Omar na kusikindikizwa na maulidi iliyofanyika nyumbani kwa Hamisa.

Advertisement

 

Aziz Ki alifuatana na baadhi ya viongozi wa Yanga wakiongozwa na Rais wa klabu hiyo Hersi Said, ambaye tangu juzi alisimamia mipango yote ya harusi kwa niaba ya wazazi wa mwanaume.

Kama ilivyo desturi Aziz Ki alivaa joho na kilemba na kushika upanga kama tamaduni zinavyotaka na baada ya kutoka msikitini waalikwa walikwenda nyumbani kwao Bahari Beach, Dar es Salaam.

Baada ya sherehe ya mahari juzi sasa imebaki sherehe ya ndoa itakayofanyika Februari 19, mwaka huu.

Hamisa amelipiwa mahari ya ng’ombe 30 katika sherehe iliyofanyika Viwanja vya gofu Lugalo, Kawe, Dar es Salaam juzi

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *