Moto utawaka Yanga v Simba

DAR ES SALAAM; MWAMUZI Amin Mohamed Omar wa Misri aliyetangazwa kuchezesha mechi ya watani Yanga v Simba Jumatano wiki hii Uwanja wa Benjamin, Mkapa Dar es Salaam, ana historia pia kuchezesha mechi za miamba hiyo dhidi ya timu za mataifa mengine katika michuano inayoandaliwa na CAF.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali kwenye mtandao, alichezesha mechi ya kwanza Robo Fainali Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini iliyofanyika Uwanja wa Mkapa na timu hizo kutoka 0-0.

Pia mwamuzi huyo alichezesha mechi ya Horoya v Simba nchini Guinea msimu uliopita, ambapo Simba ilifungwa bao 1-0 hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mwamuzi huyo atasaidiwa na Mahmoud Ahmed Abo na Samir Gamal Saad huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Ahmed Mahrous wote kutoka Misri. Mtathimini waamuzi ni Ali Mohamed kutoka Somalia.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button