Mpogolo: Tuzo ya Rais Samia imetuheshimisha

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amesema kuwa tuzo ya ‘The Gates Global Goalkeeper’ aliyoipata Rais Samia Suluhu Hassan imeleta heshima kwa Halmashauri ya Jiji, Mkoa wa Dar es salaam na taifa zima kwa ujumla.

Mpogolo amesema hayo wakati halmashauri hiyo ilipotembelewa na ugeni katika Hospitali ya Mnazi Mmoja ukiongozwa na Rais wa Idara ya Usawa wa Jinsia kutoka Taasisi ya Bill and Melinda Gates, Dk Anitha Zaidi.

Mpogolo amesema ugeni huo ni sehemu ya kuthibitisha kuwa tuzo iliyotolewa kwa Rais Samia kuwa ni tuzo sawa kwani wameweza kushuhudia namna kina mama wanavyopokelewa na kupata huduma katika suala la uzazi, chanjo na huduma nyinginezo za kina mama.

Advertisement

“Hospitali ya Mnazi mmoja inapokea zaidi ya watu 961,000 kwa mwaka lakini pia kwa kina mama tu inapokea zaidi ya watu 400, hivyo mnaona kazi kubwa ambayo inafanywa na wataalamu wetu na wamekuja kuhushudia kuwa kilichopelekea kupata tuzo ni kweli kwani wameshuhudia hakuna vifo vya mama wala mtoto vinavyotokea,” amesema Mpogolo.

Ameongeza kuwa licha ya hospitali hiyo kupata wateja wengi lakini vifo vya mama na mtoto havipo lakini pia amesema wamepongeza Rais Samia kwa kuona huduma zote zinazotolewa kwa mama na mtoto ni bure kuanzia chanjo hadi kujifungua.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam, Dk Zaituni Hamza amemshukuru rais kwa namna  anavyoimarisha sekta ya afya kuanzia katika majengo, ongezeko la vifaa tiba, watumishi na kuwa ilikuwa ni bahati kwa wageni hao kufika katika hospitali hiyo kwani imekuwa ni heshima kwao na nchi kwa ujumla.

“Katika kitu ambacho kimewafurahisha sana ni kuona kwamba katika kipindi cha miaka miwili hakuna kifo kilihotokana na uzazi na zaidi katika hospitali hiyo huku wakishangazwa kuona na idadi kubwa ya kina maama wajawazidi wanaojifungua hapa na wanaokuja kwa ajili ya kliniki,” amesema Dk Zaituni.

Ameongeza kuwa kutokana na hatua hiyo wamefurahishwa na kuona kuwa Rais Samia anastahili tuzo hiyo kwani waligawanya kwa kupita kila kitengo kukagua utoaji wa huduma mbalimbali.

Tuzo hiyo ya ‘The Gates Global Goalkeeper’ ilitokewa mwanzoni mwa wiki hii na kutunukiwa Rais Samia ikiwa ni sehemu ya kutambua nguvu na juhudi anazozifanya katika sekta ya afya na kusaidia kupunguza idadi ya vifo vya mama na mtoto kwa kufanya maboresho mbalimbali katika sekta hiyo.

 

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *