Mradi maalumu kukabili udumavu wazinduliwa mikoa mitatu

GEITA: SERIKALI imezindua Mradi wa Kuimarisha Huduma za Lishe katika mikoa ya Geita, Iringa na Tabora ili kusaidia kupunguza changamoto za udumavu, ukondefu na utapiamulo wa watoto.
Mradi huo unatekelezwa chini ya ufadhili wa taasisi ya BWP ya nchini Uingereza kwa thamani ya dola za kimarekani milioni 2 malengo makuu yakiwa ni kuimarisha lishe na maendeleo ya watoto.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe aliongoza hafla ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika katika ofisi za mkuu wa mkoa wa Geita zilizopo mjini Geita.

Akizungumza baada ya uzinduzi huo Profesa Shemdoe ameagiza viongozi wa serikali hususani maofisa maendeleo na lishe wa halmashauri kuongeza nguvu katika mpango wa kukabiliana na tatizo la udumavu.
Profesa Shemdoe ameagiza halmashauri zote kwenye mikoa husika kuendelea kutenga kiasi cha sh 1,000 kwenye bajeti zao kwa kila mtoto wa chini ya miaka mitano ili kujenga jamii iliyo bora.

Aidha ameitaka mikoa ya Geita, Iringa na Tabora kuimarisha ufuatiliaji wa mradi jumuishi wa lishe na shughuli zote zinazotekelezwa katika jamii kwa ajili ya kukabiliana na matatizo ya lishe
Ameelekeza kuwa wakati wa mradi huo, halmashauri zihakikishe zinatoa takwimu sahihi na kwa wakati ili kuzingatia utoaji huduma sahihi kwa kuzingatia ushahidi unaotokana na takwimu.
Profesa Shemdoe amewataka viongozi kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa huduma bora za malezi ya watoto wachanga wakati wa mchana (Day Care) kuwezesha maendeleo bora ya watoto.
Amesisitiza kuwa mikoa hiyo inapaswa kuimarisha huduma za ufuatiliaji na ukuaji wa maendeleo ya watoto, ili kubaini watoto wenye hali duni ya lishe na kuwaunganisha kwenye huduma stahiki.
“Watoto wetu ndio mtaji wetu, tuwatunze vyema ili wapate lishe bora Geita bila utapiamulo inawezekana, Tabora bila utapiamulo inawezekana Iringa bila utapiamulo inawezekana”.

Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Lishe Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Luitfrid Nnally ameainisha kiwango cha udumavua mkoani Geita ni asilimia 38, Tabora asilimia 33 na Iringa asilimia 57.
Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Profesa Tumaini Nagu amesema mradi umezingatia tathimini iliyofanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) iliyobainisha changamoto hiyo ya lishe.
Mwakilishi wa taasisi ya BWP, Dr Taye Balcha amesisitiza kuwa mradi huo umezingatia tathimini ya serikali na hivo na kutambua kuwa wahanga wakubwa wa udumavu ni watoto.
Mkuu wa mkoa wa Geita, Martine Shigella ameahidi kuwa mkoa wa Geita kwa kushirikiana na mikoa inayonufaika na mradi huo watatumia fursa hiyo kupunguza kiwango cha lishe kilichopo.




This was a in point of fact real sativa gummy edibles . The ironmongery felt honest, the draw was fluent, and there weren’t any annoying clogging issues, which makes a huge difference. The flavor stayed bathe a exhaust and enjoyable without starting to cultivation burnt too with dispatch, and the drag itself looked expertly made morality alibi of the box. The total to it felt unswerving and unexcitedly to use. Seeing that anyone looking against a straightforward tote with considerate flavor and dependable mat‚riel, this one positively checks the boxes.