Mwinyi: Tuendeleze maono ya Mkapa

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema njia bora ya kuuenzi urithi wa Hayati Rais Benjamin Mkapa ni kuendelea kuwekeza katika uongozi, kuimarisha sekta ya afya na kuwawezesha vijana kushiriki katika maendeleo ya Afrika.

Dk Mwinyi amesema hayo leo Julai 16, 2026, wakati wa Jukwaa la Nne la Kuuenzi Urithi wa Mkapa na maadhimisho ya miaka 20 ya Taasisi ya Benjamin William Mkapa Foundation yaliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Amesema taasisi hiyo imeendelea kuwa mshirika muhimu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha mifumo ya afya, kuendeleza rasilimali watu wa sekta hiyo na kuboresha huduma za afya ya msingi.

Katika hafla hiyo, Dk Mwinyi alitunukiwa tuzo maalumu ya kutambua mchango wake katika maendeleo ya Taasisi ya Benjamin William Mkapa Foundation, huku Makamu wa Rais, Dk Emmanuel John Nchimbi, akimkabidhi tuzo hiyo. Aidha, Dk Mwinyi alimkabidhi Dk Nchimbi Tuzo ya Juu ya Uongozi katika Mageuzi ya Afya kwa niaba ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Mama Anna Mkapa, viongozi wa serikali, mabalozi, wadau wa maendeleo, wataalamu wa afya na wageni mbalimbali. SOMA: Rais Samia kuongeza ajira sekta ya afya

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button