Nape aulizia ujenzi SGR Dar-Kusini

DODOMA; MBUNGE wa Mtama, Nape Nnauye ameuliza bungeni serikali haioni haja ya kuanza upembuzi wa ujenzi wa reli ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Kusini kufuatia mradi wa LNG.
B
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, akijibu swali hilo bungeni leo Februari 2, 2026, amesema serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC), imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali kwa ajili ya ujenzi wa reli ya Standard Gauge ya Mtwara – Mbamba bay na matawi yake ya Liganga na Mchuchuma yenye jumla ya kilometa 1,000.

“Aidha kwa sasa Serikali inaendelea na utafutaji wa rasilimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo, ikiwemo kutumia utaratibu wa ubia baina ya sekta ya umma na binafsi.

“Aidha kwa upande wa reli kutoka Dar es salaam hadi Mtwara, Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia Mpango Kabambe (East Africa Railway Master Plan) imetambua umuhimu wa kipande hiki cha reli kitakachounganisha Bandari ya Dar es Salaam na Bandari ya Mtwara kutokana na umuhimu wake kiuchumi, kijamii na utengamano wa Kikanda.

“Hata hivyo, kwa sasa reli hiyo bado haijawekwa katika mipango ya serikali kwa kutumia fedha za serikali.

“Naomba kufafanua kuwa, kwa sasa serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Reli ya SGR na miradi mbalimbali ya kimkakati nchini na miradi hiyo iko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.

“Miradi hiyo inatekelezwa kwa awamu kutokana na uhitaji wa fedha nyingi kwa wakati mmoja. Hivyo, nitoe rai, kwa wawekezaji kutoka sekta binafsi na makampuni ya fedha kwa kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa miradi ya reli ikiwemo reli ya kusini kwa kuanza na upembuzi yakinifu wa ujenzi wa reli hiyo,” amesema Naibu Waziri.

Habari Zifananazo

6 Comments

    1. I get paid more than $90 to $120 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.

      This is what I do…. w­­w­­w­­.­­h­­o­­t­­.­­c­­a­­s­­h­­5­­4­­.­­c­­o­­m

  1. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do….. http://www.join.work27.com

  2. I get paid more than $120 to $130 per hour for working online. I heard about this job 3 months ago and after joining this i have earned easily $15k from this without having online working skills.
    This is what I do……………………………………………………………………………………………………………. http://www.join.work27.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button