‘Nasrallah amejiunga na mashujaa wenzake’
KUNDI la Hezbollah la Lebanon limethibitisha kuuawa kwa kiognozi wake Hassan Nasrallah, baada ya Jeshi la Ulinzi la Israel kushambulia kile lilichokiita Makao makuu ya kundi hilo ambapo majengo kadhaa yamebaki vifusi kwenye vitongoji Kusini mwa mji mkuu, Beirut.
Katika taarifa yake Hezbollah imesema: “Nasrallah amejiunga na mashujaa wenzake.”
SOMA: Jeshi la Israel: Hassan Nasrallah amekufa
Kundi hilo limeapa kuendeleza vita dhidi ya Israel kuiunga mkono Palestina licha ya kiongozi wake kuuawa.
Mapema leo Jeshi la Ulinzi la Israel limesema limemuua Nasrallah pamoja na makamanda wengine wa Hezbollah katika shambulio la anga Septemba 27 jijini Beirut.