MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya ligi inarejea leo ikifanyika michezo tisa katika viwanja tofauti.
Moja ya mechi za kukata na shoka ni kipute kati ya Real Madrid na Borussia Dortmund katika uwanja wa Santiago Bernabeu uliopo mji mkuu wa Hispania, Madrid.
SOMA: Utamu warejea Ligi ya Mabingwa Ulaya
Mchezo huo ni wa kisasi kwani timu hizo zilipokutana katika fainali ya Ligi ya Mabingwa msimu wa 2023/2024 Real Madrid iliibuka mshindi dhidi ya Borussia Dortmund wa mabao 2-0 na kutwaa taji.
Mechi nyingine zinazopigwa leo ni kama ifuatavyo:
Real Madrid Borussia Dortmund
AC Milan vs Club Brugge
AS Monaco vs FK Crvena Zvezda
Arsenal vs Shahtar Donetsk
Aston Villa vs Bologna
Girona vs Slovan Bratislava
Juventus vs VfB Stuttgart
Paris Saint-Germain vs PSV Eindhoven
Sturm Graz vs Sporting CP