Paroko, baba mbaroni mauaji ya Asimwe

Msemaji wa Jeshi la Polisi DCP David Misime

DODOMA – Jeshi la Polisi limesema linawashikilia watu tisa akiwemo Baba mzazi na paroko msaidizi kwa tuhuma za mauaji ya mtoto mwenye ualbino Asimwe Novart (2) wa kijiji cha Bulamula wilaya ya Muleba mkoani Kagera.

Taarifa ya Polisi imesema watuhumiwa hao walieleza jinsi walivyoshirikiana na Baba mzazi wa mtoto huyo,  Novart Venant, Desideli Evarist ambaye ni mganga wa jadi na mkazi wa Nyakahama.

Wengine waliokamatwa ni Elipidius Rwegoshora Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bugandika, ambaye anadaiwa kumfuata na kumshawishi Baba mzazi wa mtoto ili wafanye biashara ya viungo vya binadamu. 

Advertisement

“Pia anatuhumiwa kuwa ndiye aliyemtafuta mganga wa jadi na kulipia gharama zote za uganga,” imesema taarifa ya Polisi.

Watuhumiwa wengine ni Danstan Kaiza mkazi wa Bushagara, Faswiru Athuman , Gozibert Alkadi, Rwenyagira Burkadi, Ramadhani Selestine na Nurduni wote wakazi wa Nyakahama, Kamachumu.

Msemaji wa jeshi la Polisi DCP David Misime amesema washukiwa hao wamekamwatwa na viungo vya mwili vinavyo sadikiwa kuwa ni vya marehemu aliyekutwa ameuawa na mwili wake kutelekezwa kwenye karavati Juni 17 mwaka huu.

SOMA: Serikali: Tumieni kiwanda cha viuadudu Kibaha

“Polisi kwa kushirikiana na raia wema wanaochukia vitendo vya kinyama kama hivyo walianza msako mkali kuanzia Mei 31, 2024 hadi usiku wa kuamkia Juni 19, 2024 ambapo watuhumiwa tisa wamekamatwa,” amesema DCP Misime.