Patashika za EPL, Ligue 1 kuanza leo

Baadhi ya wachezaji wa Manchester United wakifanya mazoezi.

MSIMU mpya wa Ligi Kuu England(EPL) na Ufaransa 2024/2025 unaanza leo kwa mchezo mmoja kila ligi.

‘Mashetani Wekundu’, Manchester United itakata utepe EPL kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford ikikiwasha dhidi Fulham.

SOMA: Chelsea kuanza na Man City EPL

Advertisement

Bingwa mtetezi wa EPL ni Manchester City itakayoanza kampeni kutetea taji ugenini Agosti 18 dhidi ya Chelsea.

Timu zilizopanda daraja kucheza EPL ni Ipswich Town, Leicester City na Southampton.

Kunako Ligue 1, bingwa mtetezi Paris Saintt-Germain itaanza kampeni kutetea taji ugenini dhidi ya Le Havre.

Timu zilizopanda daraja kucheza Ligue 1 ni AJ Auxerre, Angers SCO na AS Saint-Étienne.

Katika Ligi Kuu Hispania iliyoanza Agosti 15, leo zitapigwa mechi mbili ambapo Celta Vigo itakuwa wenyeji wa Deportivo Alaves wakati Sevilla itakuwa ugenini dhidi ya Las Palmas.