TETESI za usajili zinasema Tottenham Hotspur imekubaliana na Bayern Munich dili la pauni milioni 50 kwa ajili ya kumsajili fowadi wa kifaransa Mathys Tel. (L’Equipe – in French)
Hata hivyo, Manchester United inapanga kumuuza winga wa Argentina mwenye umri wa miaka 20, Alejandro Garnacho, na kumsajili Tel kwa mkopo (Independent).
Tel anapenda kuhamia Old Trafford kuliko Arsenal, Chelsea na Tottenham, na anasubiri kuona kama nia ya Manchester United ina manufaa kabla ya kufanya uamuzi. (i Sport)
Al-Nassr inapanga kutoa ofa ya pili na ya mwisho kwa ajili ya kumsajili winga wa Brighton na Japan mwenye umri wa miaka 27, Kaoru Mitoma, yenye thamani ya pauni milioni 90. (CBS Sports)
Mshambuliaji wa Paris Saint-Germain na Hispania, Marco Asensio, mwenye umri wa miaka 29, ni mmoja wa washambuliaji ambao Aston Villa in nia kuwasajili kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Mail)
Aston Villa pia inafikiria kutoa dau kwa mshambuliaji wa Wolves mwenye umri wa miaka 25, Matheus Cunha raia wa Brazil. (Guardian)