TIMU ya Polisi Tanzania imeita mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono kuelekea mchezo wa Ligi ya Championship dhidi ya Kiluvya United utakaochezwa katika Uwanja wa Ushirika Moshi, Februari 9.

Ofisa habari wa Polisi Tanzania Inspekta Frank Lukwaro amesema kikosi cha timu hiyo kinaendelea na mazoezi ili kuhakikisha kuwa kinapata alama tatu katika uwanja wake wa nyumbani.
“Ili timu ipate matokeo mazuri inahitaji mashabiki wengi wajitokeze kwa wingi kutoa hamasa kwa wachezaji wapate morali ya kupambana uwanjani, tunawahimiza mashabiki zetu waje kwa wingi,”amesema.
Mpaka sasa timu ya Polisi ipo nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi ya Championship ikiwa na alama 20 baada ya kucheza michezo 17.