QATAR kufadhili Jeshi la Lebanon

DOHA : SERIKALI ya Qatar imetangaza mpango wa kutoa ruzuku ya dola milioni sitini kufadhili mishahara ya jeshi la Lebanon pamoja na kutoa magari kadhaa ya kijeshi.
Tangazo hili limetolewa wakati wa ziara rasmi ya Rais wa Lebanon, Joseph Aoun, aliyetembelea Doha. SOMA: Hezbollah yatangaza ushindi
Ruzuku hii inatarajiwa kusaidia vikosi vya Lebanon kudumisha utulivu na kudhibiti mipaka ya nchi hiyo, hasa baada ya kusitishwa kwa mapigano kati ya Hezbollah na Israel mnamo mwezi Novemba. Qatar inaweka juhudi kubwa katika kusaidia nchi za Kiarabu katika kukabiliana na changamoto za usalama na utulivu katika mkoa huo.



